• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na nchi mbalimbali za Afrika zaanzisha ushirikiano wa kupambana na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-04-03 20:14:02

    Rais Joao Manuel Goncalves Lourenco wa Angola ametoa wito kwa Waangola kujifunza uzoefu na nidhamu ya wachina.

    Rais Lourenco amesema hayo baada ya kuona video moja ya kujifunza uzoefu wa China katika kupambana na virusi vya Corona iliyopigwa na mwanafaunzi wa Angola anayesoma mjini Xiamen China.

    Waziri wa mambo ya ndani ya Angola Bw. Pedro Sebastiao amesema, mafanikio ya China katika kupambana na virusi hivyo yameipa dunia muda wa kujiandalia na kutoa uzoefu mzuri. Angola inaishukuru kwa msaada wake na inatarajia pande hizo mbili zitaendelea kuimarisha ushirikiano wa kupambana na virusi hivyo.

    Habari nyingine zinasema, kampuni ya China imetoa vifaa vinne vya kufanya mkutano kwa njia ya video kwa Ghana. Waziri wa afya wa Ghana Bw. Kwaku Agyemang-Manu ameishuruku kampuni hiyo kwa msaada wake. Amesema, uzoefu wa China katika kupambana na virusi hivyo utaongoza mpango wa Ghana katika vita hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako