• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Virusi vya Corona vyaenea katika nchi 50 za Afrika

    (GMT+08:00) 2020-04-03 20:14:22

    Takwimu zilizotolewa na Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika zimeonyesha kuwa, hadi kufikia jana, nchi 50 barani humo zilitangaza kuwa na kesi 6,470 za maambukizi ya virusi vya Corona, na idadi ya vifo imefikia 241.

    Kenya imetangaza kuwaacha huru wahalifu 4,800 ambao wanatumikia kifungo cha chini ya miezi 6 ili kupunguza hatari ya maambukizi ya virusi hivyo gerezani.

    Somalia jana pia imetangaza kuwaacha huru wafungwa 148 waliokutwa na makosa madogo.

    Nayo Benki ya maendeleo ya Afrika imetangaza kutoa msaada wa dola za Marekani milioni 2 katika kukinga mlipuko wa virusi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako