• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kesi za maambukizi ya virusi vya Corona zafikia laki 8.9 duniani

    (GMT+08:00) 2020-04-03 20:14:39

    Ripoti iliyotolewa na WHO imeonyesha kuwa, mpaka kufikia saa nne jana kwa saa za Ulaya ya Kati, idadi ya kesi za maambukizi ya virusi vya Corona imefikia 896,450 na idadi ya vifo imefikia 45,526 duniani, huku kwa bara la Ulaya, idadi ya maambukizi imefikia 503,006 na vifo 33,604.

    Taasisi ya Kukinga na Kudhibiti Magonjwa ya Robert Koch nchini Ujerumani imetangaza kuwa, kuvaa barakoa (mask) kunaweza kupunguza kwa ufanisi maambukizi ya virusi vya Corona na kushauri watu wote kuvaa mask katika maeneo ya umma.

    Aidha, mwenyekiti wa kamati ya Ulaya Bibi Ursula von der Leyen amesema, kamati hiyo itaanzisha mfuko wa fedha kiasi cha Euro bilioni 100 kuwasaidia wafanyakzi kudumisha kipato na makampuni kuendelea na uzalishaji. Bibi Leyen pia amesema, wakulima na wavuvi pia watasaidiwa. Kamati hiyo imechukua hatua kuharakisha manunuzi ya vifaa vya matibabu na kuhakikisha usafirishaji wa mizigo kutoka nchi za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako