• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuongeza misaada kwa Afrika katika kukabiliana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-04-03 20:45:48

    Rais Xi Jinping wa China ameahidi kuongeza misaada kwa Afrika katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona.

    Rais Xi amesema hayo leo alipozungumza na rais wa Namibia Hage Geingob. Amesema China itatoa misaada ya vifaa vya kukinga virusi hivyo kwa nchi za Afrika, pia imetoa uzoefu wake kwa nchi hizo kwa njia ya video. Ameongeza kuwa licha ya serikali, kampuni za China barani Afrika pia zimetoa misaada kwa nchi zilizoko, na kuahidi kuongeza misaada hiyo kwa Afrika.

    Rais Xi amesema, China inapenda kushirikiana na Nambia, kuendelea kuelewana, kusaidiana, na kuongeza ushirikiano halisi, ili kuhimiza uhusiano kati yao na kati ya China na Afrika uwe wa kiwango cha juu zaidi.

    Kwa upande wake, rais Geingob amesema, rais Xi ameonesha uhodari wake kwa kuwaongoza Wachinda kushinda virusi vya Corona, ikiwa rafiki mkubwa zaidi wa Namibia na Afrika, China imetoa misaada yenye thamani kubwa kwa nchi za Afrika wakati wa janga la COVID-19.

    Huu ni mwaka wa 30 tangu China na Nambia zianzishe uhusiano wa kibalozi. 

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako