• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakanusha madai kuwa kuna wafungwa zaidi ya milioni moja wa Kiislamu nchini humo

    (GMT+08:00) 2020-04-03 20:46:41

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hua Chunying amekanusha madai kuwa kuna wafungwa zaidi ya milioni moja wa Kiislamu nchini humo, na kusema China inawataka baadhi ya wanasiasa wa Marekani kuacha kutoa kauli zisizo za kweli na kutilia maanani mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

    Hua amesema hayo baada ya Balozi asiye na ubalozi wa Marekani anayeshughulikia mambo uhuru wa kuabudu Sam Brownback kudai kuwa, China imewafunga watu wengi kutokana na sababu ya kidini, wakiwemo Waislamu zaidi ya milioni moja.

    Hua amesema madai hayo sio ya kweli, kwani serikali ya China inalinda uhuru wa kuabudu wa wananchi wake, na kwamba nchini China hakuna wafungwa wa kidini. Ameongeza kuwa, China hivi sasa ina watu karibu milioni 200 wanaoabudu dini mbalimbali, na kati yao milioni 20 ni Waisalamu. Amesema mkoani Xinjiang kuna misikiti elfu 24.4, ambapo kila Waislamu 530 wana msikiti mmoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako