• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafanya maombolezo ya kitaifa kutoa rambirambi kwa waliofariki kutokana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-04-04 10:52:12

    Viongozi wa China wamejiunga na wananchi kote nchini katika shughuli ya maombolezo ya kitaifa leo Jumamosi, kutoa rambirambi kwa mashujaa na ndugu waliofariki dunia kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

    Leo bendera zinapepea nusu mlingoti kote nchini na kwenye balozi za China katika nchi za nje, na shughuli zote za burudani pia zimesitishwa. Kuanzia saa nne asubuhi, rais Xi Jinping, viongozi wengine wa China na wananchi wote walikaa kimya kwa dakika tatu, huku ving'ora, honi za magari, treni na meli zikiapigwa kote nchini.

    Watu 14 waliojitoa muhanga kwenye mstari wa mbele wa mapambano dhidi ya virusi vya Corona, wakiwemo madaktari, wauguzi, polisi na wafanyakazi wa mitaani, wamepewa sifa ya Mashujaa wa Taifa.

    Mlipuko wa virusi vya Corona ni tukio la dharura linalohatarisha afya ya umma, ambapo virusi vilienea kwa kasi zaidi na kwenye sehemu nyingi zaidi, na pia ni vigumu zaidi kudhibitiwa tangu Jamhuri ya watu wa China ilipoanzishwa.

    Hadi kufikia Aprili 3, watu 3,326 wamefariki kutokana na virusi vya Corona nchini China, wakiwemo wafanyakazi 46 wa afya. Kwa mujibu wa wataalamu, uenezi wa virusi hivyo kimsingi umezuiliwa na kudhibitiwa nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako