• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema haiwezi kukaa bila kufanya chochote wakati nchi za Ulaya zinaathiriwa na janga kubwa la virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-04-04 18:49:59

    China imetoa salamu za pole kwa Umoja wa Ulaya na nchi wanachama wake walioathiriwa na janga la virusi vya Corona, na kusema ni kupitia ushirikiano tu, jamii ya kimataifa inaweza kushinda janga hilo.

    Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi ameyasema hayo alipoongea kwa njia ya simu na mkuu wa sera za kidiplomasia na usalama wa Umoja wa Ulaya Josep Borrel. Bw. Wang amesema hivi sasa Umoja wa Ulaya unatumia nguvu zote kupambana na virusi vya Corona, na licha ya kukabiliwa na hatari ya kuibuka tena kwa maambukizi ya virusi hivyo ndani ya nchi, China inapenda kutoa misaada kwa Umoja wa Ulaya na nchi wanachama wake kulingana na mahitaji yao.

    Amesisitiza kuwa China na Ulaya ni wenzi wa kimkakati kwa pande zote, na China haiwezi kukaa bila kufanya chochote wakati rafiki yake ana taabu, sembuse kutoa msaada kwa lengo binafsi. Ameongeza kuwa ushirikiano wa kupambana na virusi vya Corona haupaswi kusumbuliwa na itikadi tofauti, shutuma zisizo na msingi na hata kuingiliwa na mambo ya kisiasa.

    Bw. Borrel ameishukuru na kuipongeza China kwa kutoa msaada kwa nchi za Ulaya na kufanya kazi za kiujenzi katika vita dhidi ya virusi vya Corona duniani. Amesema kutoa msaada kwa nchi zenye mahitaji ni utamaduni wa China, na Ulaya inapenda kushirikiana na China katika vita hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako