• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yaanzisha kipindi cha mafunzo ya redio kufuatia mlipuko wa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-04-05 18:54:54

    Bodi ya Elimu ya Rwanda REB imeanzisha kipindi cha mafunzo kwa njia ya Redio ya shule za msingi kufuatia kufungwa kwa taasisi za elimu kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona nchi humo.

    Kwa mujibu wa REB, somo la kwanza lilitangazwa jana Jumamosi kwenye redio ya taifa ya Rwanda likihusisha kusoma na kuandika kwa shule za msingi.

    Masomo yatakayofuata yataendelea Jumatatu ambayo yatahusu lugha rasmi ya Rwanda Kinyarwanda na Kiingereza. Mkurugenzi mkuu wa REB Irenee Ndayambaje amesema kipindi hicho kitasaidia wanafunzi kuendelea na masomo wakati wakiwa nyumbani, akisisitiza kuwa masomo muhimu yatapewa kipaumbele. Walimu watafundisha masomo taratibu kuhakikisha wanafunzi wanajifunza na kuelewa vizuri wakiwa nyumbani na kwamba kila somo litachukua dakika 20 hadi 30.

    Serikali ya Rwanda imefunga taasisi za elimu Machi 14 baada ya nchi hiyo kuthibitisha mgonjwa wa kwanza wa COVID-19.

    Habari nyingine zinasema kikundi kimoja cha dini chenye watu zaidi ya 65 magharibi mwa Rwanda walikamatwa Jumamosi kwa kukiuka amri ya kukaa ndani baada ya kukusanyika kwa ajili ya sala. Meya wa Wilaya ya Karongi Mkoa wa Magharibi Vestine Mukarutesi amesema kikundi hicho kilikamatwa kwenye nyumba ya mfuasi mmoja walikokuwa wamejikusanya kwa ajili ya kusali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako