• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump asema Marekani itakuwa na vifo vingi vinavyotokana na ugonjwa wa Corona siku chache zijazo

    (GMT+08:00) 2020-04-05 18:56:26

    Rais Donald Trump wa Marekani amewaambia Wamarekani kuwa tayari kwa ongezeko kubwa la vifo vinavyotokana na ugonjwa wa virusi vya Corona katika siku kadhaa zijazo, wakati nchi hiyo inakabiliwa na kitu anachokiita kuwa ni wiki mbili ngumu za janga la kimataifa la virusi vya Corona.

    Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Ikulu ya White House, rais Trump alisema "Marekani itaingia katika hali ya kutisha zaidi, ambapo kutakuwa na vifo vingi sana, idadi ambayo huenda Marekani iliwahi kushuhudia tu katika Vita Vikuu vya Kwanza na Vya Pili Vya Dunia."

    Serikali ya Marekani ilisema inapanga kupeleka maelfu ya wanajeshi kwenye majimbo kusaidia kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona, wakiwemo elfu moja kwenda mjini New York.

    Rais huyo pia alipuuza ukosoaji unaosema kuwa serikali kuu haijafanya vizuri kugawa mashine za kusaidia kupumua kwa majimbo yenye wagonjwa wengi mahututi, akisema baadhi ya magavana wanaomba mashine nyingi kuliko wanazohitaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako