• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Sekta ya utalii yaomba kutotozwa ushuru

    (GMT+08:00) 2020-04-06 18:56:09

    Bodi ya utalii nchini Uganda inaiomba serikali ya kitaifa kuwaondolea ushuru washika dau wote katika sekta hiyo ili waweze kukabiliana na hali ngumu iliyopo kwa sasa, kutokana na virusi vya corona.

    Mojawapo ya mapendekezo ya bodi hiyo, ni kusongesha mbele muda wanaopaswa kulipa ushuru, kwa angalau mwaka mmoja. Aidha wanaomba kupunguziwa asilimia 40 kwa matumizi mengine ya kimsingi, haswa wenye hoteli.

    Kwa mujibu wa Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Utalii nchini Uganda Bi Lilly Ajarova, sekta hiyo imepata pigo kubwa sna na huenda ikapoteza zaidi ya dola bilioni 1.6 mwaka huu, kwa sababu ya virusi vya corona.

    Sekta ya Utalii nchini humo imeajiri takriban waganda laki tano, na ilikuwa ikitarajia ukuaji wa angalau asilimia 10 mwaka huu. Hata hivyo, mlipuko wa virusi vya corona umewaathiri pakubwa, ikizingatiwa kwamba hakuna mtalii yeyote anayeruhusiwa kuingia nchini hivi sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako