• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Pato la Ndani Rwanda lakua

    (GMT+08:00) 2020-04-06 18:56:34

    Taasisi ya Taifa ya Takwimu Rwanda (NISR), imesema pato la ndani la Taifa (GDP) Rwanda, limekua kwa asilimia 9.4 mwaka jana kufikia faranga bilioni 105.

    Kwa mujibu wa taasisi hiyo, sekta kubwa za uchumi ni kilimo kwa asilimia 24, viwanda kwa asilimia 18, huku huduma zikichangia kwa asilimia 49 . Kodi za bidhaa zilichangia kwa asilimia tisa.

    Kuhusu ukuaji wa sekta, kilimo kilikuwa kwa asilimia tano, viwanda asilimia 16, huku huduma ikikua kwa asilimia nane.

    Katika viwanda, ukuaji wake umechangiwa na ujenzi kwa asilimia 33 na uzalishaji kwa asilimia 11.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako