• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya mpito ya Sudan kulazimika kuendelea na mpango wa ruzuku

    (GMT+08:00) 2020-04-07 17:32:34

    Serikali ya mpito ya Sudan inaweza kulazimika kuendelea na mpango wa ruzuku wenye utata baada ya mkutano uliopangwa kuhusu uchumi kushindwa kuanza kutokana na janga la coronavirus.

    Mkutano huo ungetoa maagizo ya kisheria na maamuzi juu ya maswala ya msaada wa bidhaa, sera za kifedha, viwango vya kubadilishana, hali ya sekta ya benki, mambo yanayohusiana na sera za pensheni na uchumi mkubwa, na pia njia za kurejesha fedha zilizoporwa kutoka kwa serikali iliyopita.

    Ruzuku ya bidhaa ni moja wapo ya mipango yenye utata, ambayo inachukua zaidi ya dola milioni 300 kila mwaka kama njia ya kusaidia watu masikini kutoka kwa bei kubwa ya chakula.

    Tayari, nchi inakabiliwa na uhaba wa bidhaa za kimsingi kama mafuta, unga wa ngano, gesi ya kupikia na dawa zingine kwa sababu ya kukosekana kwa fedha za kigeni, na kutokana na kukosekana kwa usawa katika biashara kwa zaidi ya dola bilioni 4. Sasa, janga limeharibu mipango yote ya uokoaji.

    Waziri wa Fedha wa Sudan Ibrahim al-Badawi amesema kuwa nchi hiyo itaathirika zaidi kiuchumi na janga la Corona.

    Waziri huyo amesema kwamba wizara yake itatoa msaada wa pesa taslimu wenye jumla ya pauni milioni 210 ya sudan ($ 379,5752) kwa vikundi vilivyoathiriwa na kufungwa kwa biashara zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako