• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Uganda iko katika hali ngumu ya kifedha .

    (GMT+08:00) 2020-04-07 17:32:57

    Wizara ya Fedha na serikali kwa ujumla wametumia wiki kadhaa kukusanya maoni na kuzingatia mielekeo ya jinsi ya kukabiliana na mzozo wa uchumi ambao umeletwa na mlipuko wa virusi vya corona.

    Rais Museveni ametaka kupunguza athari mbaya zinazoweza kuzuka kwa uchumi, akisema sekta kama utalii na ukarimu zimeathirika sana, na zingine kama kilimo na utengenezaji zinaweza kustawi.

    Serikali tayari imefanya hatua kadhaa katika mikutano yao, sana sana kupitia Benki ya Uganda, ikiangalia mabenki ya biashara ili kuhakikisha kuwa wanabaki sawa na wanauwezo wa kusambaza pesa ili uchumi uendelee.

    Waziri wa fedha wa Uganda Bw Kasaija ameandika katika jukwaa la mtandao wa kijamii kuwa Serikali iko katika hali ngumu ya kifedha .

    Ameendelea kusema Uchumi unajivuta kwa sababu virusi vya corona. Ukusanyaji wa ushuru umeenda chini kando na ile walitarajia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako