• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki kuu ya Uganda imepunguza kiwango kikubwa cha riba kwa asilimia 8 kutokana na virusi vya corona.

    (GMT+08:00) 2020-04-07 17:33:23

    Benki kuu ya Uganda ili punguza kiwango cha sera yake kwa pointi 100 za msingi hadi asilimia 8 kusaidia uchumi ambao umepigwa na athari ya milipuko ya virusi vya corona.

    Benki hiyo pia imesema inatarajia ukuaji wa uchumi "kupungua sana", kati ya asilimia 3 hadi 4 kwa mwaka wa fedha hadi Juni, kutoka kwa makadirio ya awali ya asilimia 5.5-6.

    Sekta kama vile utengenezaji, burudani na biashara zilikuwa zikichukua pigo kubwa kutoka kwa usumbufu unaosababishwa na coronavirus na kuwalazimisha kurekebisha makadirio ya ukuaji, benki imesema.

    Kiwango cha riba cha benki sasa ni cha kiwango cha chini kabisa tangu serikali ilipoleta sera ya fedha inayolenga mfumko wa bei mwaka 2011.

    Kiwango hicho kilikuwa cha asilimia 9 tangu Oktoba wakati kilikatwa kutoka asilimia 10.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako