• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Carrefour yapata ongezeko la mauzo la asilimia 28

    (GMT+08:00) 2020-04-08 18:50:30

    Maduka ya Carrefour yanayomilikiwa na wawekezaji wa Ufaransa yamerekodi mauzo yenye thamani ya Shilingi bilioni 18.7 nchini Kenya mwaka jana.

    Mmiliki wa kipekee wa biashara ya Carrefour nchini Kenya Majid Al Futtaim, imetangaza ongezeko la mauzo ya asilimia 28 kutoka shilingi bilioni 14.6 bilioni mwaka 2018.

    Carrefour imesema tangu kuzinduliwa nchini Kenya miaka minne iliyopita, imepata ukuaji wa haraka zaidi kuliko ilivyotarajiwa kuvutia wateja wengi hasa wenye mapato ya wasatani.

    Sasa Carrefour imetangaza mipango ya kuendeleza upanuzi wa biashara zake katika masoko muhimu ikiwemo Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako