• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Wafanyabiashara katika Soko la Soroti waajiri walinzi kusaidia wateja kuosha mikono

    (GMT+08:00) 2020-04-08 18:52:03

    Wafanyabiashara katika Soko Kuu la Soroti nchini Uganda wameajiri walinzi ili kusaidia ili kuhakikisha wateja wote wanaosha mikono yao kabla ya kuingia sokoni humo.

    Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara wa Soko la Soroti Bwana George William Eriebat, alisema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia wasiwasi kwamba baadhi ya wateja walikuwa wanakaidi agizo la kunawa mikono ikiwa ni hatua ya kuzuia kuendea kwa virusi vya korona.

    Mkuu wa Wilaya ya Soroti, Bwana William Wilberforce Tukei, aliwapongeza wachuuzi katika soko la Soroti kwa mpango huo. Kama kwenye nchi nyingi barani Afrika Uganda imechukua hatua kadhaa za kukabili corona ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku usafiri.

    Hata hivyo Rais wan chi hiyo Yoweri Museveni ameendelea kuonya wafanyabiashara wanaopandisha bei za bidhaa wakati huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako