• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SADC kuruhusu kuendelea usafirishaji wa bidhaa muhimu

    (GMT+08:00) 2020-04-08 18:52:21

    Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), limeridhia usafirishaji wa bidhaa muhimu kupita katika mipaka ya nchi zilizo katika jumuiya hiyo bila kuathiri afya za madereva na watu waliopo mipakani

    Mawaziri hao ni wa mambo ya nje, fedha, viwanda na biashara, utalii, mambo ya ndani pamoja na uchukuzi kutoka nchi 16 wanachama wa jumuiya hiyo.

    Mawaziri hao walikutana Dar es Salaam kwa kikao cha dharura na kuainisha bidhaa hizo kuwa ni chakula, vifaa tiba, dawa, mafuta, makaa ya mawe, pembejeo za kilimo, vifungashio pamoja na bidhaa zote zinazohusika katika utengenezaji, uchakataji na uhifadhi wa chakula.

    Vilevile, wameazimia kuzuia usafirishaji usio wa lazima wa abiria kupitia mipakani na vile vile kuratibu sera, kanuni na hatua za haraka za kitaifa za kukabiliana na ugonjwa wa corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako