• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sekta ya Utalii Zanzibar yaathirika,hoteli zafungwa

    (GMT+08:00) 2020-04-09 19:21:42
    Hoteli za kitalii katika eneo la mji Mkogwe visiwani Zanzibar zimefungwa kwa muda usiojulikana kutokana na kukosa wageni pamoja na kujiepusha na corona.

    Corona imesababisha wageni wengi waliokuwa wamejiandaa kwenda kutembelea vivutio mbalimbali, kuahirisha safari zao na haijulikani hali hiyo itakwisha lini.

    Ofisa mtendaji wa Hoteli ya Park Hayat, Nicolas Sedour, alikiri kufungwa kwa hoteli yake ya kitalii iliyopo pembezoni mwa bahari ya Hindi, ambayo wateja wake wengi ni watalii kutoka katika nchi mbalimbali.

    Alisema baada ya kufungwa kwa huduma mbalimbali, wamepanga kufanya matengenezo madogo katika hoteli hiyo.

    Hoteli za Tembo na Dhow Palace ziliopo jirani na Hoteli ya Park Hayatt, nazo pia zimefungwa.

    Athari za corona zimewalazimisha wahudumu wa hoteli hizo kuzifunga kutokana na ukosefu wa wageni.

    Baadhi ya hoteli sasa zinatumia fursa hiyo kufanya matengenezo madogo ili kujitayarisha na msimu wa utalii ambapo utategemea zaidi kumalizika kwa janga la corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako