• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Kenya yapendekeza kuongeza bei za bidhaa

    (GMT+08:00) 2020-04-09 19:21:59
    Serikali ya Kenya imetoa mapendekezo ya kuongeza bei ya dawa,petroli,maziwa,mkate pamoja na bidhaa nyingine muhimu.

    Kwenye mswada ambao umeandaliwa, gesi ya kupikia sasa itaanza kutozwa ushuru wa thamani (VAT) wa asilimia 14 na kusababisha kuongezeka kwa bei yake.

    Bidhaa nyingine ambazo zitaongezwa bei iwapo mswada wa marekebisho ya ushuru utapitishwa na Bunge ni neti za kuzuia mbu na chanjo za kuzuia magonjwa hatari.

    Wataalamu wametaja hatua hii kama kinaya kwa kuwapunguzia wananchi baadhi ya kodi na kisha kutumia mbinu nyingine kuwaongezea gharama.

    Kulingana na Rais wa Chama cha Mawakili (LSK) Nelson Havi kwenye barua kwa Karani wa Bunge la Taifa, hatua hizo zitakuwa na madhara makubwa kwa umma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako