• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara wakubwa Kampala watoa somo kwa wananchi,waokoe pesa zao na wanunue vitu vilivyo na umuhimu tu

    (GMT+08:00) 2020-04-09 19:22:25
    Janga la ugonjwa wa Korona limeathiri uchumi wa dunia na vilevile kuwa na athari mbaya kwa mapato ya watu na hali z amaisha kwa ujumla.

    Nchini Uganda wafanyabiashara wakubwa wamewasihi watu na wafanyabiashara kutafuta njia mpya za kujikimu katika kipindi hiki cha maambukizi ya ugonjwa wa korona.

    Mfanyabiashara wa Kampala,Drake Lubega amesema ipo haja kwa watu kupunguza matumizi yasiyo ya muhimu na pia kutofanya uwekezaji sehemu ambayo ni vigumu kutabiri iwapo uwekezaji huo utalipa.

    Mfanyabiashara mwengine maarufu jijini Kampala,Uganda,Bw Sudhir Ruparelia amesema watu wanafaa kujijengea tabia ya kujiuliza iwapo kitu wanachotaka kununua kama kina umuhimu wakati huu.

    Alisema watu wakijiuliza swali hilo wataepuka matumizi mabaya ya fedha kipindi hiki.

    Alisema hivi sasa nguvu zote na juhudi zote zinafaa kuelekezwa katika kujilinda na maambukizi ya ugonjwa wa korona na sio matumizi mabaya ya pesa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako