Aidha, imesema taarifa hiyo itatoa dira ya namna ya kuanzisha viwanda vikiwamo vya kusindika pamba na inatarajiwa kukamilika kabla ya Julai, 2020.
Wizara hiyo ilitoa kauli hiyo bungeni jana wakati ikijibu swali la Mbunge wa Busega (CCM), Dk. Raphael Chegeni.
Katika swali lake, Chegeni alisema zao la pamba linakabiliwa na kero nyingi kutokana na kukosekana uhakika wa bei yake.
Kwa mujibu wa majibu ya Wizara hiyo, lengo la kazi hiyo ni kukuza soko la pamba na taarifa hiyo itatoa dira ya namna ya kuanzisha viwanda hivyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |