• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • EPL: Penyenye zasema ligi inaweza kumalizwa kutokana na mlipuko wa Corona

    (GMT+08:00) 2020-04-10 08:05:02

    Mkurugenzi wa klabu ya Udinese, inayoshiriki Ligi ya Serie A, Pierpaolo Marino, amedai mabosi wa Ligi Kuu England wanajipanga tu kutoa tangazo la kumaliza msimu wa Ligi Kuu England kutokana na janga la corona kupamba moto. Mabosi wakubwa wa soka walitoa taarifa wiki iliyopita wakisema wanafikiria kumaliza msimu huu, lakini hawakuweka tarehe maalumu ya kurejea kwa mikimikiki hiyo ya soka kutokana na janga hilo la corona kuzidi kuwa kubwa zaidi. Kinachoelezwa ni kwamba mabosi hao wameruhusiwa kuendelea na ligi mwezi Juni, mechi zikichezwa bila ya mashabiki, lakini jambo hilo litafanyika kama tu kutaonekana kuna unafuu kwenye suala la maambukizi mapya ya virusi hivyo vya corona. Lakini, kwa mujibu wa bosi huyo wa Udinese, Marino ambaye klabu hiyo ina wamiliki walewale wa kutoka familia ya Pozzo inayomiliki klabu ya Watford ya Ligi Kuu England, alisema England inajiandaa kufuata nyayo za Ubelgiji za kuamua kumaliza ligi yao. Kwenye Ligi Kuu England, Liverpool licha ya kuongoza kwa tofauti kubwa ya pointi, bado hakuna uhakika kama itapewa ubingwa huo endapo ligi itatangazwa kuwa imefutwa jumla. Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Ligi Kuu England, Richard Masters alisema watapoteza kiasi kisichopunguza Pauni 1 bilioni kama ligi haitaanza tena na kuendelea kufika mwisho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako