• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa mwongozo wa kurejesha uzalishaji mali wakati wa kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-04-10 09:35:53

    Mwongozo uliotolewa na Kikundi cha uongozi cha mwitikio wa COVID-19 cha China umesema China itaendelea kurejesha uzalishaji mali kwa utaratibu kwenye msingi wa kudhibiti kwa ufanisi kusambaa kwa virusi vya Corona.

    Mwongozo huo umesema wakati wa kujilinda dhidi ya maambukizi kutoka nje ya nchi na kuzuia kuibuka tena kwa mlipuko wa virusi vya Corona nchini, idara zote na maeneo yote yanapaswa kuratibu juhudi kati ya udhibiti wa virusi na maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na kuharakisha mchakato wa kurejesha uzalishaji mali na maisha ya wananchi kwenye hali ya kawaida wakati hatua za kuzuia kuenea kwa virusi zinaendelea kutekelezwa.

    Mwongozo huo umeagiza juhudi zaidi zifanywe kurejesha uzalishaji kwenye mnyororo mzima wa viwanda na sekta ya huduma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako