• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wasisitiza kuunga mkono kithabiti Shirika la Afya Duniani

    (GMT+08:00) 2020-04-10 10:41:27

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) amesema Umoja wa Afrika unapongeza kazi nzuri zinazofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika kupambana na virusi vya Corona.

    Rais Ramaphosa ametoa taarifa na kusema AU pia inashukuru usimamizi wa mkurugenzi mkuu wa WHO Bw. Tedros Ghebreyesus katika kuongoza dunia katika mwitikio dhidi ya janga hilo.

    Amesema AU inaridhika na mipango na hatua zinazoendelea kuchukuliwa na WHO kuzuia kuenea kwa virusi hivyo kama vile kuhamasisha rasilimali, kubadilishana habari sahihi na kutoa msaada wa kiufundi na vifaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako