• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ufungaji wa mipaka waathiri biashara Afrika

    (GMT+08:00) 2020-04-10 19:10:10
    Biashara barani Afrika zinaonekana kuathiriwa na ufungaji wa mipaka ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona. Usafirishaji wa bidhaa kutoka nchi moja hadi nyingine unadaiwa kuathiri kabisa biashara kutoka nchi moja hadi nyingine.Inadaiwa nchi 31 barani Afrika tayari zimefunga kabisa mipaka yake huku nyingine ikiwemo Kenya ikidaiwa kukubali tu usafirishaji wa mizigo. Wasafirishaji wa mizigo katika eneo la Afrika mashariki wanadai inawachukua muda mrefu sana kuchukua mizigo kutoka bandari ya Mombasa baada ya wafanya kazi wa idara za serikali ambazo zinatakiwa kuidhinisha uchukuliwaji wa mizigo kupunguza idadi ya wafanya kazi wakati huu wa virusi vya corona. Miongoni mwa idara hizo ni pamoja na mamlaka ya kodi, Shirika la bandari la Kenya na Shirika la biashara nchini Kenya. Mashirika mengi hivi sasa yanazuia kuzuia mawasiliano ya moja kwa moja na wateja.

    Katika bandari ya Mombasa, ushushaji wa mizigo pia umepunguzwa baada ya wasimamizi kupunguza muda wa kufanya kazi tangu marufuku ya kutotoka nje ya kati ya saa moja hadi saa kumi na moja asubuhi iwekwe na serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako