• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KENYA: KEBS KUHAKIKISHA KWAMBA MAFUNDI WANATENGENEZA BARAKOA BORA

    (GMT+08:00) 2020-04-13 17:27:24

    Shirika la Kukadiria Ubora wa Bidhaa Nchini Kenya (KEBS), limetangaza kuwa litawasaidia mafundi kote nchini ili waweze kutengeneza maski zinazotimiza viwango hitajika.

    Kwenye notisi iliyochapishwa kwenye gazeti la Daily Nation, toleo la Ijumaa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Benard Njiraini, maafisa wake wameanza kuzunguka kote nchini wakiwaelekeza mafundi kuhusu namna ya kutengeneza maski hizo za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.

    Hakikisho la KEBS limejiri baada ya Wizara ya Afya kutoa agizo kwamba sharti watu wavalie maski hizo katika maeneo ya umma nyakati zote

    Serikali imekuwa ikihimiza kampuni za kutengeneza nguo na mafundi wa nguo kutengeneza vifaa hivyo kwa wingi ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

    Hii ni baada ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kutoa kuthibitisha kuwa kuvalia maski ni njia mojawapo ya kuzuia watu kuambukizwa virusi hivyo ambavyo vinaweza kusalia hewa kwa zaidi ya saa tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako