• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ZANZIBAR: MAGOFU ZANZIBAR YATUMIKA KUTANGAZA UTALII.

    (GMT+08:00) 2020-04-13 17:29:56

    Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itatumia utajiri wa magofu ya kale ya kihistoria yaliyopo Zanzibar, kwa ajili ya kutangaza na kukuza sekta ya utalii nje ya nchi.

    Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Mahmoud Thabit Kombo, anasema mikakati ya wizara ni kuimarisha magofu ya kale kuwa moja ya sehemu ya utalii utakao wawezesha wageni kujua historia ya Zanzibar na watawala.

    Alizitaja faida za kufanyika kwa ukarabati wa magofu ya kale, ni kutoa fursa kwa watalii na wageni mbalimbali kutembelea Zanzibar, na kupata maelezo ya historia ya mambo ya kale kwa ajili ya kufanya utafiti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako