• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ETHIOPIA: SHIRIKA LA NDEGE LA ETHIOPIA LAWAPA LIKIZO YA LAZIMA WAFANYIKAZI WAKE.

    (GMT+08:00) 2020-04-13 17:30:20

    Shirika kubwa la ndege barani Afrika, Ethiopian Airlines, imeanza kuwafuta kazi wafanyikazi wake baada ya sekta ya usafiri wa ndege kuathirika pakubwa na mlipuko wa virusi vya corona.

    Hatua ya kuwafuta baadhi ya wafanyikazi, na kuwapa wengine likizo ya lazima imejiri baada ya shirika la ndege la Ethiopia kupata shinikizo la kufutilia mbali safari zake za ndege kwa mataifa mengi ambayo yamekumbwa na virusi vya corona. Ikumbukwe kwamba, mataifa mengi duniani hivi sasa hayaruhusu usafiri wa ndege nje na ndani ya mataifa hayo, kama njia moja ya kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona.

    Wanaofutwa kazi kwenye shirika la ndege la Ethiopia, ni wale ambao mikataba yao ilikuwa ya muda. Wale waliokuwa wameajiriwa, wamepewa likizo ya lazima ya siku 90, bila malipo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako