• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Burundi: Serikali ya fungua mipaka yake ya Rwanda, DR Congo kwa ajili ya usafirishaji ya mizigo.

    (GMT+08:00) 2020-04-14 19:34:36

    Serikali ya Burundi imefungua tena mipaka yake kwa usafirishaji wa bidhaa kutoka Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya wiki mbili za kufungwa kwa mipaka ya kaskazini na magharibi mwa nchi hiyo.

    Burundi illipofika Machi 30,imezuia rasmi malori yote ya kubeba mizigo kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitisha kupitia Rwanda.

    Kufuatia kuzuiwa kwa mizigo, Rwanda iliarifu Kenya na Uganda kwamba haitaruhusu malori ya kubeba mizigo ya Burundi kutoka nchi hizo mbili za Afrika Mashariki.

    Rwanda ilifanya uamuzi huo baada ya malori kadhaa kukwama kwa upande wa Rwanda, pamoja na bidhaa zao.

    Mara mara nyingi, bidhaa zinazopitia kuenda Burundi hutoka bandari ya Kenya ya Mombasa.

    Jana usiku, serikali ya Burundi ilisema "licha ya kufungwa kwa mipaka ya kaskazini na magharibi na Rwanda na DRC, usambazajio wa bidhaa utaendelea.

    Serikali ya Burundi imeambia Madereva wa lori waheshimu hatua zilizochukuliwa ili kupambana na kuenea kwa virusi vya corona.

    Hivi sasa Mipaka yote iko wazi, Malori yenye kubeba mizigo itaendelea na oparesheni zake kulingana na miongozo ya EAC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako