• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wazalishaji wakubwa wa mafuta ulimwenguni wamekubaliana kupunguza kiwango cha uzalishaji mafuta kwa takribani mapipa milioni 10 kwa siku

    (GMT+08:00) 2020-04-14 19:35:00

    Wazalishaji wakubwa wa mafuta ulimwenguni wamekubaliana kupunguza kiwango cha uzalishaji mafuta kwa takribani mapipa milioni 10 kwa siku ili kuidhibiti bei iliyoporomoka kutokana na janga la kirusi cha corona.

    Waziri wa Mafuta wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Abdulaziz bin Salman Al-Saud na mwenzake wa Urusi, Alexander Novak wakiongoza kikao cha OPEC mwezi Disemba 2019.

    Katika mkutano wao kwa njia ya vidio wazalishaji hao wa shirika la OPEC linalotawaliwa na Saudi Arabia na washirika wao wanaoongozwa na Urusi waliafikiana kukata 10% ya kiwango cha kawaida cha uzalishaji, ingawa katika uhalisia linaweza kufikia hadi asilimia 20.

    Kwa mujibu wa Waziri wa Nishati wa Mexico, Rocio Nahle, mataifa hayo yalikubaliana kuwa kuanzia mwezi Mei, yatazalisha mapipa milioni 9.7 ya mafuta kwa siku, chini kidogo ya mapipa milioni 10 iliyokuwa imezungumziwa awali.

    Waziri wa Nishati wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Abdulaziz bin Salman, ambaye aliongoza mkutano huo kwa kushirikiana na mawaziri wenzake wa Urusi na Algeria, alithibitisha kuwa mjadala wao wa siku nne ulimalizika kwa maridhiano.

    Saudi Arabia inasema huenda punguzo hilo likakata uzalishaji wa mapipa milioni 12.5 kwa siku, kwa sababu ya kiwango kikubwa cha uzalishaji kutoka nchi hiyo.

    Rais Donald Trump wa Marekani aliyapokea makubaliano hayo aliyoyaita mazuri kwa yote, na ambayo yataokowa maelfu ya ajira kwenye sekta ya nishati nchini mwake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako