• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Kagame aeleza matumaini ya kufufuka kwa uchumi

    (GMT+08:00) 2020-04-15 19:02:37

    Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema kuwa uchumi wan chi hiyo utaanza kufanya vyema tena baada ya dunia kukabili kabisa virusi vya Corona.

    Kagame ameyasema hayo wakati akizungumza kwa njia ya video na wawekezaji wa Afrika chini ya mwavuli wa Invest Africa.

    Invest Africa ni jukwaa la kibiashara linalokuza biashara na uwekezaji barani humo.

    Kwa jumla lina kampuni wanachama 400 zikiwemo za kimataifa, taasisi za kifedha, mitaji binafsi, wajasiriamali na mashirika ya kiserikali.

    Rais Kagame aliwahahakikishia wawekezaji kuwa licha ya kupungua kwa ukuaji kwenye sekta mbalimbali za uchumi bado kuna matumaini makubwa ya kurejea kwa ukuaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako