• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watengezaji bidhaa Uganda waandika mapendekezo ya kuimarisha sekta hiyo,wataka serikali kuwaunga mkono

    (GMT+08:00) 2020-04-16 19:29:00

    Baada ya kukusanya maoni kutoka kwa wanachama 1,400,watengenezaji bidhaa chini mwamvuli wa Chama cha Watengezaji Bidhaa cha Uganda (UMA) ,wameandika mapendekezo wanayosema yatasaidia kuimarisha sekta hiyo kutokana na athari za ugonjwa wa Corona.

    Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kupunguza vikwazo vya upatikanaji wa malighafi,ulipaji wa madeni ya ndani,mikataba mipya ya ulipaji madeni na urejeshwaji wa kodi ya thamani.

    UMA inasema mapendekezo hayo yatasaidia kupiga jeki uchumi na pia kuruhusu biashara kuwa na mtiririko wa fedha.

    Hatua nyengine kulingana na UMA ni pamoja na kupunguza kiwango cha Benki Kuu ili kuchochea mikopo ya sekta binafsi,kukuza sera ya Nunua vya Uganda Jenga Uganda,kurekebisha ushuru wa umeme mwaka mzima na kuondoa ushuru wa mapato na malipo ya uzeeni.

    Hata hivyo UMA imesema kuwa serikali na watengezaji bidhaa wanafaa kulenga kuhusu fursa zilizojitokeza kutokana na ugonjwa wa Corona.

    Miongoni mwa fursa hizo,UMA imesema ni sekta uuzaji nje haswa sekta ya chakula na bidhaa nyingine zilizotengenezwa ambazo serikali inafaa kusaidia ili kujenga uwezo mkubwa wa uuzaji nje bidhaa katika kanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako