• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Zanzibar kujenga kiwanda cha mwani Pemba

    (GMT+08:00) 2020-04-16 19:29:39
    Serikali ya Zanzibar imesema, inakusudia kujenga kiwanda cha kusarifu mwani na kuongeza thamani ya zao hilo huko Chamanangwe kisiwani Pemba katika mwaka wa fedha 2020-2021.

    Hayo yalisemwa na Waziri wa Biashara na Viwanda, Balozi Amina Salum Ali, wakati akitoa ufafanuzi na kujibu hoja za Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa kamati ya Fedha Biashara na Kilimo ya mwaka 2019-2020.

    Balozi Amina alisema hizo ni sehemu za juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Zanzibar katika kuona kilimo cha mwani kinakuwa mkombozi kwa wananchi wa Unguja na Pemba.

    Alizitaja juhudi hizo ni pamoja na kuwawezesha wakulima wa kilimo cha mwani kupiga hatua kubwa ya maendeleo na uchumi pamoja na kutafuta soko la uhakika nje ya nchi.

    Alisema mafanikio yameanza kuonekana kwa wakulima wa mwani kwa kupanda kwa bei ya zao hilo kutoka Sh.400 hadi kufikiya Sh.1,800 kwa kilo moja.

    Aidha, alisema Serikali itaendelea kuweka mipango madhubuti ili kukifanya kilimo cha mwani kuwa cha manufaa ya kibiashara na kubadilisha maisha ya wananchi wanaoishi pembezoni wa mwambao wa pwani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako