• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TPSF yafurahishwa na wakulima wa mboga

    (GMT+08:00) 2020-04-17 18:45:31
    Taasisi ya Sekta Binafsi nchini Tanzania (TPSF) imesema imefurahishwa na ubunifu wa Chama cha Wakulima wa Mboga na Maua (TAHA) kwa kufanya makubaliano ya kusafirisha moja kwa moja bidhaa zao wakati huu ambapo dunia napitia wakati mgumu cha ugonjwa wa corona.

    Chama hicho kimeingia katika makubaliano na Shirika la Ndege la Ethiopia kusafirisha moja kwa moja matunda, mboga na maua.

    Mwenyekiti wa TPSF, Angelina Ngalula, amepongeza makubaliano hayo na kusema ni mfano wa kuigwa wa ubunifu unaochangia sana kuimarisha uchumi wa Tanzania na wa dunia wakati huu.

    Aidha ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuunga mkono juhudi za wananchama wa TPSF, na kuziomba taasisi katika sekta ya usafirishaji kutoa huduma kwa ufanisi ili kupunguza gharama kusudi Tanzania inufaike na mkataba ambao umefikiwa. Ameziomba kongani nyingine za TPSF kubuni mikakati ya kuwasaidia wafanyabiashara kuendelea kuwa na kipato.

    Alitaja majukumu matatu ya wanachama wa TPSF wakati huu ni kutoa elimu ya kuzuia maambukizi, kulinda ajira na kuhakikisha huduma muhimu kama upatikanaji wa vyakula na zingine zinaendelea.

    Aliwataka watanzania kujikita katika kilimo hicho kwani matunda na mboga vinahitajika kwa wingi ndani na nje ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako