• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UWABIMIDO Watakiwa kuwa wabunifu kuongeza mitaji

    (GMT+08:00) 2020-04-17 18:46:28
    Umoja wa Wafanyabiashara Minadani (Uwabimido) umetakiwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea, ili waweze kukuza mitaji yao.

    Ofisa wa masoko wa Jiji la Dodoma, James Yuna, ametoa ushauri huo alipokuwa akizungumza na viongozi wa umoja huo wa wafanyabiashara wa minadani Mkoa wa Dodoma.

    Yuna alisema ili kwenda na kasi ya biashara zao wanatakiwa kutofanya biashara zao kwa mazoea, na kuhakikisha wanafikia malengo ya kuinua mitaji yao kukuza kiuchumi na hatimaye kuwa wafanyabiashara wakubwa.

    Aliwataka kuepukana na migogoro isiyo na tija ambayo mara nyingi inarudisha nyuma maendeleo yao.

    Hata hivyo, alisema wafanyabiashara wote wa minadani wanatakiwa kuwa katika eneo moja ambalo litakuwa linajulikana na kuondokana na kukaa kwenye maeneo yasiyo rasmi ambayo yanaweza kusababisha ajali kwa mali zao na wateja.

    Katika hatua nyingine, Yuna aliwataka kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kushirikiana na halmashauri husika, ikiwa ni pamoja na kufuata maelekezo na kanuni wanazoelekezwa ili waweze kufanya biashara kwa uhuru na ufanisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako