• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Maduka Easleigh yafungwa

    (GMT+08:00) 2020-04-20 16:23:49
    Wafanyibiashara wa Eastleigh, Nairobi wamefungam maduka makubwa katika mtaa huo ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.

    Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara wa Maduka makubwa mtaani humo Omar Hussein alisema walichukua hatua hiyo baada ya kubaini kuwa watu katika majengo hayo ya kibiashara huwa hawazingatia masharti ya serikali ya kutotangamana. Aidha, aliitaka serikali kuanzisha shughuli ya unyunyiziaji dawa katika barabara za mtaa huo pamoja na uzoaji taka wakati huu ambapo maduka hayo yatasalia kufungwa.

    Maduka yote ya bidhaa mbalimbali yamefungwa kuanzia Ijumaa, na yatasalia hivyo kwa muda usiojulikana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako