• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Ulanguzi biashara sukari wafichuka.

    (GMT+08:00) 2020-04-20 16:28:16
    Sasa ni wazi kwamba baadhi ya wafanyibiashara nchini Tanzania, wanashirikiana wenyewe kwa wenyewe, kufanya ulanguzi wa sukari kwa lengo la kupata faida kubwa. Hili limebainika siku mbili baada ya serikali ya Tanzania kuonya kuhusu kuongezeka kwa bei ya sukari nchini humo.

    Kwa mujibu wa jarida la Nipashe la Ijumaa iliyopita, sukari kilo moja inauzwa kwa kati ya shilingi 2,800 na 4,500 katika sehemu mbali mbali nchini humo. Hizi ni pesa za Tanzania. Aidha, Zanzibar, kilo moja ya sukari inauzwa kwa shilingi 1,800, pesa za Tanzania.

    Kutokana na hali hii, serikali kupitia kwa waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, imesema itachukuwa hatua kali za kisheria dhidi ya wafanyibiashara, watakaobainika kuficha sukari, kwa lengo la kupandisha bei wakati huu wa janga la Corona.

    Aidha Waziri amesema kwamba, serikali imeagiza zaidi ya tani 20,000za sukari nje ya nchi ikiwa ni tahadhari ya kuwa na akiba ya kutosha ya bidhaa hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako