Kampuni hizo zitatengeneza maski, magwanda ya madaktari na vizuizi vingine ili kusaidia serikali kuu kupunguza uagizaji wa bidhaa hizi kutoka mataifa ya nje.
Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa Halmashauri ya vyakula na dawa, Dkt Charles Karangwa, kampuni hizo tayari zimepewa ruhusa ya kuanza shughuli hiyo baada ya ukaguzi wa kina. Baadhi ya kampuni zilikuwa tayari zikitengeneza bidhaa hizi, ila bila idhini. Lakini kwa sasa, wamepewa fursa hiyo kuendelea na kazi hiyo. Kwa jumla, kampuni hizi zinatarijwa kutengeneza takriban maski 600,000 kila siku.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |