• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Shule za kibinafsi zinageukia darasa za mtandaoni

    (GMT+08:00) 2020-04-21 19:36:41
    Shule za kibinafsi zinageukia darasa za mtandaoni ili kupata mapato kutoka kwa ada watakaotoza, lengo kuu ni kupigania kubaki katika soko, licha janga la virusi vya corona ambalo limesababisha kufungwa kwa taasisi za masomo.

    Uchumi ukiendlea kusikia athari za ugonjwa wa corona, kuna hofu kwamba shule nyingine za kibinafsi zinaweza tolewa kwa biashara kutokana na kupoteza chanzo kikuu cha mapato karo.

    Shule za kibinafsi kama vile Braeburn, Aga Khan, Banda, Cavina, wamefikia makubaliano na wazazi kutoza ada ya kufundisha wanafunzi mtandaoni.

    Hii itaongeza mtiririko wa fedha zao na kuwezesha kulipwa mishahara kwa walimu na wafanyikazi wasio wafundishaji, na ulipaji wa mikopo kwa wawekezaji ambao wamechukua mkopo wa benki ili kujenga au kupanua shule zao.

    Shule za kibinafsi zimeonya uwezekano wa shida ya kifedha na waalimu wao na wafanyikazi kusimamishwa kazi kama janga la corona ulimwengu litaendelea zaidi ya Aprili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako