• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDI: Mabondia Okolla na Achieng kupanda ulingoni Agosti

    (GMT+08:00) 2020-04-22 15:39:34

    Bondia wa uzito wa juu ama heavyweight Morris Okolla ama Hercules na bondia wa uzito wa lightweight Sarah Achieng watapanda ulingoni dhidi ya waponzani wao watakaotajwa baadaye kugombea taji la Umoja wa Ngumi wa Afrika (ABU) na Baraza la Ngumi la Commonwealth (CBC) mwezi Agosti mwaka huu. Mwenyekiti wa Tume ya Ngumi za Kulipwa ya Kenya (KPBC) Reuben Ndolo amesema, mapambano hayo yalipangwa mwezi uliopita lakini yaliahirishwa kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona. Mabondia hao wawili watapigana na wapinzani ambao watajulikana baada ya janga la Corona kumalizika. Ndolo pia amesema, aliyekua mshikizi wa taji la super bantamweight la Baraza la Ngumi la Dunia kwa wanawake Fatuma Zarika Iron Lady na Nick Mwangu ama Makavelli pia watashiriki katika mapambano ya utangulizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako