• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Van Persie afichua kilichomuondoa Arsenal

    (GMT+08:00) 2020-04-22 15:41:22

    Aliyekua nahodha na mshambuliaji Arsenal Robin Van Persie, amefichua siri ya kuachana na klabu hiyo yenye maskani yake makuu kaskazini mwa jijini London, na kutimkia Manchester United mwaka 2012. Taarifa za awali zilieleza mshambuliaji huyo aliondoka Arsenal, baada ya kushindwa kuafikiana na uongozi wa juu kuhusu maslahi ya mkataba mpya, ambao alihitaji ufungamane na vipengele vya kusajiliwa wachezaji wenye hadhi ya kuipa mataji The Gunners. Hii leo Van Parsie ambaye tayari ameshastaafu soka, amefichua siri na kueleza uvumi huo haukuwa kweli, kwani wakati huo alitamani kuendelea kuitumikia Arsenal ambayo ilimtazama kama mtetezi kwenye nafasi ya ushambuliaji. Gwiji huyo kutoka nchini Uholanzi amesema taarifa zilizotolewa wakati ule zilikua kinyume chake, kwani viongozi wa Arsenal waligoma kumpatia mkataba mpya na ndio maana alifanya maamuzi ya kuondoka. Amesema mpaka hii leo hakuna yoyote aliyekua nafahamu ukweli wowote, huku akitangaza dau kwa mdau yoyote mwenye ushahidi kama alikataa kusaini mkataba mpya ajitokeze na atamzawadia pesa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako