• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Mkutano wa 26 wa Jumuiya ya Madola wahirishwa

    (GMT+08:00) 2020-04-22 19:54:32
    Mkutano wa 26 wa Jumuiya ya Madola uliopangiwa kuanyika baadaye baadaye mwaka huu nchini Rwanda umeahirishwa kutokana na virusi vya corona.

    Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola imesema mkutano huo wa kilele ulipangiwa kufanyika kuanzia Juni 22-27.

    Mkutano huo ulitarajiwa kuhudhuriwa na wakuu wa nchi 52, pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na mwakilishi wa Malkia, Prince Charles.

    Rwanda pia ikiwa nchi mwenyeji ilitarajia kusaini mikataba ya biashara ya zaidi ya dola milioni 700 wakati wa mkutano huo.

    Hoteli pia zilitarajiwa kufaidika na zilikuwa zimetenga angalau vyumba 8,000 vya wajumbe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako