Akizindua mpango huo waziri wa kilimo Peter Munya alisema lengo la serikali ni kuboresha uzalishaji na ubora wa kahawa nchini humo ambayo imekuwa ikipungua kwa kasi.
Programu hiyo itafadhiliwa na mkopo kutoka Benki ya Dunia na baadaye inatarajiwa kufikishwa kwenye maeneo yote yanayokuza kahawa.
Awamu ya kwanza ya mradi huo itawalenga wakulima wa kaunti za Machakos, Kiambu, Muranga, Kirinyaga, Nyeri, Embu, Meru na Tharaka Nithi.
Uzalishaji wa kahawa nchini Kenya kwa sasa ni tani 40,000 na serikali inatarajia kuongeza uzalishaji hadi tani 100,000 kila mwaka.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |