• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakenya wengi wapoteza ajira kufuatia janga la Corona

    (GMT+08:00) 2020-04-30 19:43:02
    Wakenya 133,657 wamepoteza ajira baada ya kuenea kwa mlipuko wa janga la Corona.

    Haya yameelezwa katika Ripoti iliyotolewa mbele ya Kamati ya Bunge inayoonyesha kuwa janga la Corona bado linaendelea kuathiri vyanzo vya mapato vya kampuni nyingi.

    Sekta zilizoathirika mno uchukuzi,anga,hoteli na utalii,viwanda,kilimo na sekta isiyo rasmi.

    Ripoti hiyo iliyotayarishwa na Wizara ya Leba na Usalama wa Kijamii,inaonyesha kuwa ajira zote 133,657 zilizopotea ziko katika sekta rasmi.

    Aidha Ripoti hiyo inasmea kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka kutokana na kuwa makampuni mengi bado hayajaijulisha Wizara kuhusu watu waliowasimamisha kazi kama inavyohitajika chini ya Sheria ya Uajiri ya mwaka 2017.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako