• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uzalishaji kahawa Tanzania waongezeka

    (GMT+08:00) 2020-04-30 19:43:28
    Uzalishaji wa kahawa nchini Tanzania katika kipindi cha miaka minne umeongezeka hadi kufikia tani 214,962.

    Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Kilimo nchini humo Japhet Hasunga jijini Dodoma wakati akizungumzia mafanikio yaliyopatikana katika uzalishaji wa zao hilo na kusema kwa wastani kila mwaka zimekuwa zikizalishwa tani 51,777 za kahawa nzuri, hivyo kuliwezesha taifa kuingiza fedha nyingi za ndani na za kigeni.

    Pia alisema katika kipindi hicho, wakulima wamejipatia Sh. trilioni 1.195 ambazo zimewanufaisha kwa namna mbalimbali.

    Alifafanua kuwa kwa wastani baada ya kuanza kwa uandikishaji wa wakulima kwa lengo la kuwatambua ili kuwahudumia mpaka sasa wakulima 286,397 wamesajiliwa.

    Kuhusu ajira, alisema kahawa imechangia ongezeko la ajira za watu kutoka milioni 2.3 hadi milioni 2.7 ambao wamejiajiri au wameajiriwa kupitia kilimo cha kahawa na wanashiriki kwenye uzalishaji na mnyororo wa thamani.

    Pia alisema mchango wa zao hilo katika uchumi wa taifa kwenye sekta ya viwanda limechangia kiwango viwanda takribani 554 ambavyo vinajishughulisha katika uchakataji kutoka katika ngazi ya uzalishaji mpaka ulaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako