• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waagizaji mafuta ya Petroli Rwanda wasalia na mamilioni ya lita za bidhaa hiyo

    (GMT+08:00) 2020-04-30 19:43:45
    Waagizaji wa mafuta ya petroli nchini Rwanda wamesalia na milioni za lita za bidhaa hiyo kufuatia kushuka kwa hitaji kutokana na amri ya kutokuwa nje.

    Amri hiyo imepooza uchukuzi na uzalishaji wa kiviwanda na kuwaacha waagizaji wakiwa na gharama za ziada katika ada za uchukuzi na upakiaji.

    Katibu Mtendaji wa Chama cha Waagizaji wa Mafuta ya Petroli nchini Rwanda,Joseph Akumuntu amesema waagizaji wa waliagiza mafuta hayo miezi miwili kabla ya mlipuko wa Corona.Na wakati yalipofika hapa,amri ya kutotoka nje ilikuwa tayari ishaanza kutekelezwa.

    Akumuntu anasema hiyo inamaanisha vituo vya kuhifadhia mafuta vimejaa kwa sababu viwango vya matumizi vimepungua kwa asilimia 80.

    Aidha Akumuntu alisema makubaliano kati ya waagizaji na makampuni ya kusafirisha mafuta yanaeleza kuwa muagizaji atatozwa ada ya $100 kwa siku iwapo atachelewa kuchukua mzigo wake.

    Akumuntu anasema wanaishinikiza serikali kuwapunguzia kodi ambayo itawaruhusu kushusha bidhaa zao katika vituo vya kibinafsi.

    Kabla ya janga la Corona,waagizaji walikuwa wakihifadhi mafuta yao katika vituo maalum,ambapo kuna Mamlaka ya Mapato ya Rwanda katika vituo hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako