• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bei ya samaki yashuka Zanzibar kufuatia ugonjwa wa Corona

    (GMT+08:00) 2020-04-30 19:44:01
    Bei ya samaki imeshuka kwa kiwango kikubwa katika diko la Kihinani Ngalawa visiwani Zanzibar baada ya hoteli nyingi za kitalii kufungwa kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.

    Awali diko hilo lilikuwa likipokea kili 5,000 za samaki kwa siku na sasa imeshuka hadi kilo 2,000.

    Baadhi ya wafanyabiashara ambao walikuwa wakipeleka samaki hotelini na kuchuuza mitaani wamesema kushuka kwa bei ya samaki kumetokana na kuzorota kwa shughuli za utalii Zanzibar.

    Utaratibu wa kujikinga na maradhi ya Corona umezingatiwa katika madiko ya Mazizini na Kizingo visiwani humo.

    Baadhi ya wavuvi wanasema wamesimamisha shughuli zao za kwenda kuvua ili kuepuka misongamano ndani ya vyombo wanapokwenda kuvua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako