• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali yaombwa kuingilia kati kisa biashara kudorora

    (GMT+08:00) 2020-05-01 18:55:52
    Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) mjini Dodoma Ringo Iringo, imeitaka serikali kuzungumza na taasisi za kifedha zinazotoa mikopo kwa wafanyabiashara, kusimamisha ulipaji wa marejesho au kupunguza riba wakati huu ambapo ugonjwa wa corona unaendelea kuathiri biashara mbalimbali nchini humo.

    Akizungumza na wanahabari, Ringo amesema mlipuko wa ugonjwa wa corona umeathiri wafanyabiashara wote, hali ambayo inatishia hatima yao kutokana na wengi wao kuendesha shughuli zao kwa mikopo kutoka taasisi mbalimbali za fedha.

    Alisema ili kuwasaidia wafanyabiashara waliofunga biashara zao kutokana na kudorora kwa uchumi duniani, serikali hainabudi kukutana na taasisi za kifedha nchini ili kuona namna bora ya kuwasaidia.

    Aidha, alisema kuwa kama serikali itaweza kukutana na taasisi za kifedha na kujadiliana namna bora ya kuwasaidia wafanyabiashara, hatua hiyo itawasaidia kuwapunguzia msongo wa mawazo walio nao hivi sasa, kutokana na wengi wao kuendesha biashara zao kwa mikopo.

    Vilevile, aliziomba mamlaka za mapato za mikoa nchini humo kupitia mameneja wa mikoa kukutana na viongozi wa jumuiya za wafanyabiashara kujadilina namna ya kuikabili hali hiyo wakati huu wa ugonjwa wa covid 19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako