• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kahawa haina ruzuku ya mbolea'

    (GMT+08:00) 2020-05-01 18:56:51
    Wabunge wa Tanzania wameelezwa kuwa zao la kahawa nchini humo halina ruzuku ya mbolea kutokana na serikali kusitisha utoaji wa ruzuku kwa mazao ya kilimo mwaka 2016/17.

    Hayo yalielezwa bungeni na Wizara ya Kilimo wakati wa kujibu swali la kutaka kujua sababu za zao hilo kutokuwa na ruzuku ya mbolea kutoka serikalini.

    Wizara hiyo mesema kuwa ilisitisha utoaji wa ruzuku katika mazao ya kilimo, ikiwemo kahawa tangu mwaka 2016/2017 na kuachia wakulima suala la kuagiza na kununua kwa kuzingatia uwezo na uhitaji wa mnufaika kwa bei zilizo sokoni kwa wakati huo.

    Ilifafanua kuwa serikali inatambua umuhimu wa mbolea katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, likiwamo zao hilo.

    Ilieleza kuwa katika kuboresha mfumo wa upatikanaji na usambazaji wa pembejeo za kilimo hususan mbolea kwa wakulima wa mazao yote nchini, serikali ilibadilisha utaratibu wa ruzuku kwa wakulima.

    Wizara hiyo ilisema ilianzisha mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (Fertilizer Bulk Procurement System-FBPS) ulioanza kutumika msimu wa 2017/2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako