• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Dunia-Uchumi wa Kenya kuinuka mwaka wa 2021

    (GMT+08:00) 2020-05-01 18:57:09
    Benki ya Dunia imesema uchumi wa Kenya unatarajiwa kuanza kuimarika tena mwaka ujao kwa asilimia 5.2 . Benki ya dunia imesema ukuaji huo utatokana na uwekezaji mwingi katika sekta ya kibinafsi na nafasi nzuri ya daraja baada ya msukosuko wa janga la corona.Hali nzuri ya hali ya anga pia inadaiwa huenda ikapiga jeki sekta ya kilimo na kutoa matokea mazuri na shughuli za uzalishaji , usafirishaji bidhaa nje pamoja na uimarikaji wa mapato ya matumizi.Hata hivyo benki hiyo imesema ukuaji huo utategemea hatua na sera ambazo serikali itakumbatia katika kukabiliana na janga la Corona. Hatua za kukabiliana na ugonjwa wa Corona zimekuwa na athari kubwa sana katika uchumi wa Kernya jambo ambalo wachambuzi wanaona huenda likakatiza ukuaji wa uchumi wa Kenya mwaka huu. Miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kufungwa na kumbi za burudani ambazo zimeathiri uzalishaji na matumizi kote nchini Kenya.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako